MAGUFULI::MARUFUKU SAFARI ZA NJE
Rais Dk. John Magufuli, ameanza kutekeleza kaulimbiu yake ya “Hapa kazi tu” kwa kutangaza kufuta safari zote za nje ya nchi kuanzia jana kwa watendaji wa umma hadi hapo atakapolitolea maamuzi mengine suala hilo.
Aidha, amesema kama kutahitajika ulazima wa kusafiri nje, kibali lazima kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi.
Kufuatia maamuzi hayo, amesema shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi na watendaji wa umma, sasa zitafanywa na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi nje.
Dk. Magufuli, alitoa uamuzi huo ikiwa ni siku moja tu baada ya juzi kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya Fedha na kukuta baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wakiwa nje ofisi.
Uamuzi huo aliutoa jana baada ya kufanya kikao na Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa
Dk. Magufuli katika kikao hicho kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, aliwaeleza viongozi hao mwelekeo wa serikali yake anayoitaka, baada ya kuapishwa kwake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika kikao hicho, Dk. Mgufuli ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili mawaziri atakaowateua waweze kuyasimamia bila kukosa.
Mambo ambayo watendaji hao wanatakiwa kuanza kuyawekea mikakati kwa utekelezaji ni pamoja na kuanzia mwezi Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada.
Wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu, Dk.Magufuli aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa rais, atahakikisha kuanzia mwakani elimu kuanzia chekechea hadi kidato cha nne inatolewa bure.
Aidha, katika maagizo hayo, Dk.Magufuli alitaka suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi.
Aliwataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania na kwamba kama kutahitajika ulazima kwa mtumishi wa umma kusafiri nje kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi.
“Nataka serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘Hapa kazi tu’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja,” alisema Dk.Magufuli.
Dk. Magufuli katika kikao hicho alitoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji wa serikali kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kimaendeleo na kwa ufanisi zaidi.
Alimwagiza Kamishna wa TRA, Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi zinatatuliwa kama alivyoahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.
Aliitaka TRA kuhakikisha inakusanya mapato hayo kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote iliyopo nchini.
Alisisitiza kuwa katika serikali yake mtu wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais, ama Makamu wa Rais.
Alisema suala la manunuzi limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuiibia serikali kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo katika jamii.
“Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja,”alisema.
Dk.Magufuli aliwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo na maadili mema ya kazi.

NIPASHE

No comments: