RAIS MAGUFULI AFUTA SHEREHE ZA DESEMBA 9
RAIS wa Tanzania, John Magufuli anatarajia kusitisha maadhimisho sherehe za Uhuru za mwaka huu badala yake kutumia siku hiyo kusafisha mazingira kutokana na nchi kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali, Barozi Ombeni Sefue amesema kuwa sherehe hizo zinazofanyika kila mwaka Desemba 9, kuwa haitakuwa yenye shamlashamla za zinazoifanya serikali kutumia fedha nyingi na baadala yake kutumia siku hiyo kwa taifa zima kwa kusafisha mazingira ili kuondokana na vimerea vya ugonjwa huo.
Balozi Sefue amesema fedha ambazo zitatumika katika sherehe hizo ziwekwe kwenye mipango mingine ya kiserikali pamoja na siku hiyo kutafanyika usafi wa mazingira nchi nzima.
Amesema kuwa maadhimisho hayo yanaigharimu serikali kiasi cha fedha ambacho hakuwa tayari kuweka wazi na kusitisha kwa sherehe hizo kutokuwa kiasi hicho.
Balozi Sefue ameagiza kwa viongozi mbalimbali wa halmashauri, miji na majiji kuhakisha kuwa watu kwenye mamlaka zao wanashirirki kwenye zoezi hilo.
Sherehe hizo zinazofanyika kila mwaka Desemba 9 kutokana na siku hiyo nchi ya Tanzania ilitwaa Uhuru wake kutoka mikononi mwa wakoloni wa kiengereza.
MWANAHALISI

No comments: