Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

TAARIFA YA NEC YA MGAWANYO WA VITI MAALUM BUNGENI


Kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(b) na Ibara ya 78 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 86A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, Tume imepewa Mamlaka ya kutangaza Viti Maalum vya wabunge wanawake visivyopungua asilimia 30 ya wabunge wote.

Kwa mujibu wa uamuzi wa serikali wa mwaka 2010 idadi ya wabunge wanawake wa Viti Maalum iliongezwa na kufikia asilimia 40. 

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Viti Maalum ni 113 kutokana na kuwepo kwa majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi. Mgawanyo wa Viti Maalum kwa sasa ni 110. Viti 3 vilivyobaki, vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.

Vyama ambavypo vimekidhi vigezo hivyo vya Kikatiba na Kisheria vya kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge ni:

CCM viti 64

CHADEMA viti 36

CUF viti 10

No comments: