Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

MOTO WA MAGUFULI WATUA TANESCO WAFANYAKAZI 7 WASIMAMISHWA KAZI

Uongozi wa Shirika la Umeme nchini, TANESCO umewafukuza kazi wafanyakazi saba waandamizi wa shirika hilo kutokana na makosa mbalimbali yakikiwemo vitendo vya wizi, kudai rushwa, ubadhirifu wa mali wa shirika hilo pamoja na kutoa lugha chafu kwa wananchi jambo ambalo ni kinyume na taratibu za maadili ya kazi na uongozi huo kuwaonya wafanyakazi wengine wenye tabia kama hizo kwamba watachukuliwa hatua.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Mhandisi Felichesmi Mramba akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema uamuzi huo umechukuliwa ikiwa ni mpango endelevu wa shirika hilo wa kuimrisha nidhamu kwa wafanyakazi wake, kutambua wajibu wao wa kutoa huduma ya nishati kwa wananchi na siyo kuwasumbua wateja. Ametaja wafanyakazi hao wamefukuzwa ikiwemo ngazi ya mameneja, wahandisi na wahasibu kutoka mikoa ya Kinondini Kaskazini, Katavi, Kagera na Ilala.

Pia, Mramba ametoa siku saba kwa wateja ambao wanalihujumu shirika la umeme kwa kujiunganishia umeme kwa wizi kujisalimisha wao wenyewe kutokana na kuanza kwa operesheni maalumu ya nyumba kwa nyumba kuhakiki mita ili kubaini upotevu wa nishati ya umeme inayotumika bila kulipiwa.  Mpango huo utahusisha jeshi la polisi katika kuwakamata wahalifu wote na mali zao na endapo wa watashindwa kulipa faini, zitanadiwa.

Pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi Mkuu huyo amesema mpango wa uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo vya gesi tangu mwezi wa Septemba mwaka huu umesaidia kuongeza megawati 300 kutoka megawati 260 hivyo hatua hiyo imechangia kuboresha hali ya umeme hapa nchini.Amesema kuwa kuna matarajio ya kupata MW 700 ifikapo mwezi Januari mwakani kutoka kwenye umeme wa nishati ya gesi.

No comments: