Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

MAKONDA AWATANGAZIA WAENDESHA BODABODA NEEMA

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na waendesha bodaboda leo na kuahidi kushugulikia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa vikwazo vya wao kuingia katikati ya jiji.
Aidha, amewaahidi kuwapatia pikipiki kwa marejesho ya  Sh25,000 kwa wiki  kwa muda maalum kabla ya kuwaachia kabisa.
Kwa mantiki hiyo, Makonda amewataka kufanya usajili upya na kusajili vituo vyao ili watambulike kisheria huku akisema atawapatia mavazi maalum 'reflectors' kama utambulisho.
Awali, mmoja wa waendesha bodaboda hao, Daud Laurian alimsomea RC Makonda risala iliyoainisha matatizo yao ikiwemo zuio la kuingia katikati ya jiji kutokana na agizo la aliyekua  mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick Machi 3, 2014.
Waendesha bodaboda hao wamemhakikishia Makonda kuwa raia wema katika suala zima  la  ulinzi iwapo Jeshi  la  Polisi Kanda Maalum litawachukulia kama ndugu zao na marafiki. 
MWANANCHI

No comments: