Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

CHADEMA WASUBIRI AMRI YA MWISHO

Wakati wanachama, wafuasi na wapenzi wa Chadema wakitangaza utayari wa kushiriki maandamano na mikutano ya hadhara iliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia Septemba Mosi, uongozi wa chama hicho Mkoa wa Kigoma haujaanza maandalizi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Shaaban Madede alisema hawajapanga wala kuratibu maandamano hayo hadi chama kitakapotoa maelekezo.
“Sisi (Kigoma) tunafanya kila jambo la chama kwa maelekezo kutoka juu (viongozi wa Taifa) na tukipata ridhaa juu ya hilo hatutakuwa na njia nyingine, bali tutaandamana kikamilifu,” alisema Madede.
Alisema chama hicho kitapanga mahali pa kuanzia maandamano na yatakapoishia.

MWANANCHI

No comments: