Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

POLISI KUWACHUKULIA HATUA ORIGINAL COMEDY KWA KUTUMIA SARE ZAO

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kuwachukulia hatua kundi la kisanii la “ Original Comedy” kwa kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba ameeleza kuwa wanatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.
“Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.” 

 MWANANCHI

No comments: