WALIMU WANNE NA WANAFUNZI WANANE WASHIKILIWA UCHOMAJI SHULE MOTO
Walimu na wanafunzi hao, wametajwa katika kura za siri zilizopigwa na kutokana na kuibuka matukio ya kuchomwa moto shule wilayani Monduli ambapo ndani ya mwezi mmoja shule tatu zimechomwa moto na kusababisha hasara ya Sh 215 milioni.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta akizungumzia walimu na wanafunzi hao alisema majina yao yanahifadhiwa wanahojiwa na polisi ili kujua kama wamehusika na uchomaji wa shule hiyo.
MWANANCHI

No comments: