MAJALIWA ACHANGISHA SH1.4 BILIONI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA
Kiasi hicho ni fedha taslimu na ahadi ambazo zimetolewa na wafanyabiashara na mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini.
Miongoni mwa wafanyabishara hao ni Kampuni za GBP, Oilcom na Moil ambazo kwa pamoja zimeahidi kukarabati shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ambazo tayari zimefungwa.
Baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara wameahidi kutoa fedha taslimu, mabati, saruji, vyakula na nguo.
MWANANCHI

No comments: