WABUNGE ‘KUMWEKA KATI’ DK TULIA
Vikao hivyo vinapangwa kufanyika wakati mkutano wa nne ukianza rasmi kesho, baada ya kuahirishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu wakati wa mkutano wa Bajeti.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alieleza jana kuwa uamuzi wa kufanya vikao hivyo umefikiwa baada ya upinzani kukaa na viongozi wa dini Agosti 24 ili kutafuta suluhu ya kudumu.
“Kikao cha kwanza tutakaa kamati ya uongozi ya wabunge wa upinzani kujadili suala hilo, baadaye tutamaliza na kikao cha wabunge wote ili kubaini njia endelevu za kumaliza jambo hilo,” alisema Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
MWANANCHI

No comments: