Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

BOSI WA JAMIIFORUMS AACHIWA KWA DHAMANA

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Godfrey Mwampamba amemuachia huru, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media Limited, inayomilikiwa na mtandao wa kijamii wa Jamii Forum (JF), Maxence Melo baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.
Wadhamini hao wamesaini bondi ya Sh5 milioni kila mmoja huku mshtakiwa huyo akipewa sharti  asitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam.
Ijumaa iliyopita, Melo ambaye anakabiliwa na kesi tatu tofauti  alilazimika kurudi rumande  baada ya kushindwa  kukamilisha sharti la  dhamana.
MWANANCHI

No comments: