Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

WHO: HAKUNA UGONJWA WA ZIKA TANZANIA

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna  taarifa za ugonjwa wa zika  Tanzania na hakujawahi patikana mtoto aliyezaliwa na dalili hizo.
Hayo yamesemwa leo (Jumamosi) na Mwakilishi wa shirika hilo nchini Tanzania, Dk Grace Saguti alipozungumza na waandishi wa habari.
"WHO inafanya kazi na wizara ya afya kufatilia taarifa za magonjwa unaofanyika kila siku katika maeneo yote ya afya, na taarifa huletwa wizarani kisha tunashirikishwa ili kutoa katika tovuti yetu, nachoweza kusema hatujapata taarifa za magonjwa ambazo zinazoonyesha dalili za mgonjwa yoyote mwenye zika Tanzania," amesema  Dk Saguti.
Pia, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya ina mfumo maalum wa kupata taarifa za magonjwa na hakuna taarifa iliyoonyesha uwepo wa ugonjwa wa zika.
"Hakuna mgonjwa yoyote wa Zika Tanzania…narudia mara ya pili hakuna mgonjwa wa zika Tanzania," amesema Dk Kambi.

MWANANCHI

No comments: