Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

MCHINA ADAKWA KIA AKITOROSHA TANZANITE


Polisi wakishirikiana vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), wamemtia mbaroni raia wa China, Wenlong Yu(50) akitorosha madini ya aina ya Tanzanite kwenda China.
Akizungumza na wanahabari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema raia huyo wa China alikamatwa juzi saa 8:15 akijiandaa kusafiri kwenda Shanghai, China kwa kutumia ndege ya shirika la Qatar.
Kamanda Mutafungwa alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni fundi sanifu katika mgodi wa Laizer Kurian huko Mererani, kulitokana na maofisa wa polisi na vyombo vingine kumtilia mashaka.
Mutafungwa alisema baada ya kumtilia mashaka na polisi kumfanyia upekuzi, walimkuta na vipande vitano vya madini ya Tanzanite ambavyo thamani yake bado haijafahamika, akiwa amevificha ndani ya suruali ya Jeans aliyovaa. 
MWANANCHI

No comments: