WAFANYAKAZI WA SERIKALI ZA MITAA WALIA KUDHALILISHWA
TALGWU chenye wanachama zaidi ya 71,000 kote nchini kiliyasema hayo jana na kudai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kushuhudia matukio kadhaa yakifanywa na wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa kisiasa au kuonekana bora kwa Rais John Magufuli aliyewateua.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Rashid Mtima alisema tayari wameshawasilisha barua kwa makatibu tawala wa wilaya kwa lengo la kuanza kukusanya taarifa za matukio hayo ya udhalilishaji.
"Kwa mfano tunakumbuka lile tukio la OfIsa Ardhi aliyedhalilishwa na Makonda hivi karibuni, basin a huko kwenye halmashauri, watendaji wa Serikali za Mitaa wananyanyasika sana.
“Akikosea achukuliwe hatua lakini ni vyema kumpa nafasi kujieleza. Zipo taratibu za kufuata na siyo kutafuta ‘pupolarity’(umaarufu) kwa njia hizo,sasa tunaamini njia ya mazungumzo ni sahihi na tunategemea hali hiyo haitajitokeza tena,"alisema Mtima.
MWANANCHI

No comments: