UKWELI KUHUSU MWANAMKE ALIYEDAIWA KUFA KISHA KUFUFUKA DSM
Asubuhi ya April 18, 2017 kulisambaa taarifa za kufufuka kwa mwanamke ambaye alidaiwa kufa baada ya kugongwa na gari usiku wa kuamkia leo na kuthibitshwa kifo chake.
Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Anna mkazi wa Tanki Bovu jijini Dar es Salaam anadaiwa kugongwa na gari usiku wa April 17, 2017 siku ya Pasaka kisha kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa kweli amefariki, lakini taarifa za kifo hicho ziliposambaa ndipo zikaibuka taarifa nyingine kuwa angali hai.
Katika hali ya kustaajabisha, vijana wawili waishio mtaa mmoja na mwanamke huyo walijitokeza na kudai kuwa mwanamke huyo hakufa bali yupo hai amechukuliwa kimazingara.
NA AYO

No comments: