DALILI ZA NAPE KUHAMA CHAMA ZAANZA KUONEKANA,KUFANYA KAMA MALEMA WA AFRIKA KUSINI
Aliyekuwa Waziri wa Habari Ndugu Moses Nnauye hivi karibuni amekua mkosoaji mkuu wa serikali iliyoko madarakani ,Nape tokea atenguliwe kwenye nyadhifa ya uwaziri amekuwa akikosoa mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali huku akitumia mtandao wa tweeter kuweka jumbe mbalimbali nyingi zikiwa zenye mafumbo makali.
Hivi sasa kaweka picha ya kiongozi wa upinzani nchini Afrika ya kusini ndugu Malema.Malema alikuwa kwenye chama cha ANC kabla ya kutimuliwa na kuunda chama chake .Nape kuweka picha hiyo ya Malima kumezua maswali mengi wengine wakiona kama anaona dalili za kufukuzwa ndani ya CCM na anaweza fanya kama alivyofanya Malema ya kuunda chama chake cha upinzani.
No comments: