Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

UPINZANI WALIPUKA BUNGENI, WAIMBA WANA IMANI NA MKAPA, KIKWETE


Bunge limezizima kwa makofi baada ya hotuba ya mpango wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani.


Wabunge wa upinzani ambao ndiyo wengi waliobaki ukumbini baada ya wengi kwenda kufuatilia ripoti ya kamati ya pili ya Rais John Magufuli kuhusu usafirishaji wa makinikia.


Wabunge wamesimama na kuanza kuimba huku wakipiga makofi, marais wa awamu zilizopita; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wametajwa.


"Tuna imani na Mkaaapa...oya oya oya


Mkapa kweeeli...kweli


Kweli, kweli, kweli Mkapa.


Tuna imani na Kikweeetee...oya oya oya


Kikwete kweeli


Kweli, kweli, kweli Kikwete."


Wimbo huo umeimbwa baada ya Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde kulitaka Serikali kuileta bungeni mikataba yote ya madini ili ijadiliwe.

No comments: