DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME ZAWAPONZA ZAMBIA
Wanaume watatu nchini Zambia wamelazwa kwa makosa katika wadi ya wagonjwa wa kipindupindu baada ya kunywa dawa za asili zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo, ameiambia BBC kuwa mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu ambacho kilisababishwa na mchanganyiko wa chakula, pombe na dawa hizo za asili. ”Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa”'
BBC

No comments: