21 WANUSURIKA AJALI YA TRENI KIGOMA
Watu 21 wamejeruhiwa baada ya treni ya abiria iliyokuwa inatoka Tabora kuelekea Kigoma kupata ajali eneo la Malagarasi, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Akizungumza na MCL Digital leo Februari 28,2018 kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno amesema ajali hiyo imetokea leo mchana baada ya injini na mabehewa mawili kuacha njia na kuanguka.
“Mabehewa mawili ya abiria na injini ndiyo vimeanguka, majeruhi wapo 21 kati yao mmoja ndiye ameumia sana,” amesema Otieno.
Amesema jitihada za kuwapatia majeruhi hao huduma ya matibabu zinaendelea.

No comments: