PICHA ZA MSIBA WA MWANAMUZIKI RADIO
KUFUATIA kifo cha mwanamuziki nyota nchini Uganda, Moses Ssekibogo maarufu kama Mowzery Radio, kufariki dunia, hapa nimekuwekea baadhi za picha za matukio msibani kwa mwanamuziki huyo.
Mowzery amefariki jana akiwa katika Hospitali ya Case mjini Kampala.
Kkifo hicho kimetokea saa chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutoa mchango wa Sh. milioni 30 za Uganda kwa ajili ya matibabu ya mwanamuziki huyo.
“Uongozi wa Hospitali ya Case unathibitisha kupokea malipo ya UGX 30,000,000 kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Uganda @KagutaMuseveni. Tunamshukuru kwa mchango wake huo wa kugharamia matibabu kwa mwanamuziki nyota wa Uganda, Radio,” ilisema sehemu ya taarifa kutoka Hospitali ya Case.
Wiki iliyopita, polisi walisema walikuwa wamewakamata watu watano katika uchunguzi kuhusiana na kupigwa kwa Radio. Mowzery Radio aliyekuwa sehemu ya kundi la Radio and Weasel, alitoa vibao vikali kama vile ‘Bread and Butter, ‘Zuena’, ‘Magnetic’, miongoni mwa vingine vingi.
GB
No comments: