DC AAGIZA MRATIBU WA MAABARA AKAMATWE
Mratibu huyo, Emanuel Masondole, anatuhumiwa kuchukua boksi la vifaa hivyo kutoka halmashauri ya wilaya ya Korogwe vijijini akidai Halmashauri ya Korogwe mji anakofanya kazi kuna upungufu wa vifaa hivyo
Kaimu Ofisa wa dawa wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe Vijijini, Issa Mkwawa amesema tukio hilo limetokea Novemba 11 na vifaa hivyo vimerejeshwa juzi baada ya taarifa hiyo kusambaa.
Katika maelezo yake, mtuhumiwa amesema alifanya hivyo kwa ajili ya kuweka hifadhi ya kutosha ya vifaa hivyo isipokuwa hakueleweka kwa utetezi wake kwa kuwa alikuwa na hifadhi ya kutosha.
Hata hivyo mkuu wa wilaya amesema lazima mtumishi huyo achukuliwe hatua za kinidhamu ili kukomesha wizi wa dawa unaofanyika kwenye vituo mbalimbali vya afya.
''Vifaa hivyo ni vile vinavyouzwa kwenye maduka ya dawa na vituo vya afya, tunataka kukomesha tabia hiyo ambayo inaisababishia serikali hasara,” amesema Mtawiwa
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, boksi hilo la vifaa vya MRDT vina thamani ya zaidi ya sh6 milioni.
MWANANCHI

No comments: