RAIS MAGUFULI AZIDI KUBANA KILA KONA,WABUNGE NAO WAKIONA CHA MOTO
SIKU chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa Serikali bila kibali, safari hii kibao kimewagekia wabunge baada ya kuzuiwa kusafiri bila ruhusa maalumu, MTANZANIA imebaini.
Hali hiyo imeonekana kuwavuruga wabunge, kwani baadhi yao wamejikuta wakikwama katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kubainika kuwa hawana vibali vya kusafiri nje ya nchi.
Chanzo cha kuaminika kililiambia MTANZANIA kuwa, uamuzo huo wa Serikali umegeuka mwiba kwa wabunge ambao wengi wao wamekuwa wakisafiri reja reja kwa kutumia hati zao (Diplomatic Passport) kwa safari zao binafsi.
Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata (CCM), ni miongoni mwa wabunge waliotajwa, ambaye alijikuta akikwama Uwanja wa Ndege katika sehemu ya Watu Mashuhuri (VIP), baada ya kubainika kukosa kibali cha Bunge wala Ikulu kinachomruhusu kusafiri nje ya nchi.
“Huu uwamuzi ni mzuri sana kwani hivi sasa wabunge waliokuwa wamezoe kwenda nje ya nchi kila wakati wanabanwa na katika hili mbunge Martha Mlata ameonja rungu la Serikali.
“… mwishoni mwa wiki iliyopita alikuja hapa Uwanja wa Ndege eneo la VIP na kujikuta akikwama maana kwa sasa eneo la watu mashuhuri kuna orodha ya maofisa na wabunge wote ambao wameruhusiwa kusafiri nje ya nchi kwa vibali aidha cha Ikulu au cha Katibu wa Bunge ambaye kwa sasa hukiomba kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu,” kilisema chanzo hicho.
MTANZANIA ilimpomtafuta mbunge huyo wa viti maalumu ili aeleze kukwama kwa safari yake, alijibu kwa kifupi kwa kusema kwamba hawezi kuchaguliwa pa kwenda.
“Mnanichagulia pa kwenda? Nasema andikieni mnavyojua,” alisema Mlata huku akishindwa kukubali wala kukanusha kuhusu safari yake ilivyokwama.
MTANZANIA

No comments: