Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

KESI YA ASKOFU GWAJIMA KUSIKILIZWA SEPTEMBA 29

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itaendelea kusikiliza kesi ya kutoa lugha chafu  inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ifikapo Septemba 29 mwaka huu.
Kesi hiyo ilisimama kwa takribani  muda wa miezi minne baada ya mahakama kukataa kupokea CD iliyotolewa na upande wa mashtaka dhidi ya Askofu Gwajima kama kielelezo cha ushahidi kwa kuwa hakijakidhi vigezo na upande wa mashtaka kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Wakili wa Serikali, Jackqline Nyantori leo amemueleza Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha  kudai kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka dhidi ya uamuzi wa kuikataa  CD kuwa kielelezo cha ushahidi.
Hakimu Mkeha amesema kesi hiyo imekwisha simama kwa miezi minne haijasikilizwa  hivyo aliwataka upande wa mashtaka kueleza kama wana nia ya kuondoa rufaa hiyo ili kuruhusu kesi kuendelea kusikilizwa ama la.
 MWANANCHI

No comments: