MBOWE ATUPIWA VIRAGO NJE
Agosti 24, Mkurugenzi wa NHC, Nehemiah Mchechu alisema wadaiwa sugu akiwamo Mbowe wataondolewa kwenye majengo ya shirika hilo iwapo watashindwa kulipa madeni wanayodaiwa baada ya kupewa notisi ya mwezi mmoja.
Inadaiwa kuwa Mbowe kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels Limited (MHL), ilikodi jengo la NHC alilokuwa akilitumia kwa biashara ambalo linadaiwa kuwa na limbikizo la deni la Sh1.2 bilioni.
Jana kuanzia saa 1.30 asubuhi, NHC chini ya madalali wake iliwasili eneo lilipo jengo hilo ili kutekeleza uamuzi huo wa kumuondoa mmiliki huyo kwa kutoa nje vitu vilivyokuwa ndani ya ofisi za Free Media ambayo huchapisha gazeti la Tanzania Daima.
MWANANCHI

No comments: