PADRI AOMBA SERIKALI IPIGE MARUFUKU ‘VIROBA’
Mkurugenzi wa kituo cha wagonjwa na wasiojiweza cha Bashay wilayani Mbulu mkoani Manyara, Padri James Amnaay ametoa wito huo leo alipokabidhiwa msaada wa vyakula, nguo na sabuni na UWT Mbulu katika maadhimisho ya miaka 40 ya CCM.
Padri Amnaay amesema endapo Serikali itapiga marufuku pombe hizo, vijana wengi hawatajiingiza kwenye ulevi huo unawasababisha wakithiri katika ulevi huo na kuwafanya wawe vichaa.
Amesema kutokana na urahisi wa kubwebwa na bei nafuu, pombe hizo za karatasi zimewaathiri vijana wengi wanaokunywa na kulewa kisha kujiingiza kwenye dawa za kulevya na kuwasababishia kuwa vichaa.

Kweli kabisa
ReplyDeletehahahahahahahah nilijua tu
Delete