Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

MWAKYEMBE: WIMBO WA NAY WA MITEGO RUKSA


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, ameondoa zuio la kufungiwa kwa wimbo wa ‘Wapo’ wa mwanamuziki Nay wa Mitego.


Akizungumza na waandishi mjini Dodoma leo, Waziri Mwakyembe alimtaka mwanamuziki huyo auboreshe wimbo huo na ikiwezekana aende Dodoma ili akamuongezee maneno zaidi.


Kabla ya kauli ya Dk Mwakyembe ya kuondoa zuio hilo, Baraza la Sanaa la Taifa(Basata) lilizuia kupigwa au kusikilizwa kwa wimbo huo.


Jana msanii huyo alikamatwa akiwa Morogoro katika shughuli zake za muziki na kuletwa jijini Dar es Salaam, kwa kile kilichoelezwa kuwa wimbo wake umeikashfu serikali.


==>>KAMA HUJAUPAKUA HUU HAPA CHINI



No comments: