SOPHIA JUMA AONGOZA TAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA
Sophia Juma, mwanafunzi wa St Marry Mazinde Juu ya Tanga ameibuka kidedea katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai 15, akishika namba moja kitaifa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde imeeleza kuwa nafasi ya pili imeshikwa pia na msichana, Agatha Julius Ninga wa Tabora Girls. Wote walikuwa wakichukua masomo ya mchepuo wa Sayansi (PCB).
Kadhalika taarifa hiyo imeeleza kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).
Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.
“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11 umepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;
“Pia ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”
Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.

No comments: