Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

AJALI YA TAHMEED” MKOANI TANGA..MMOJA AFARIKI DUNIA,20 WAJERUHIWA

index
Baadhi ya majeruhi wakiokolewa kutoka katika ajali hiyo ya basi la Tahmeed.

Basi la kampuni ya Tahmeed limepata ajali baada ya kupinduka eneo la Kitumbi Kata ya Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga na taarifa za awali zinasema ajali hiyo imesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 20 kujeruhiwa wakati dereva wa basi hilo akimkwepa mwendesha pikipiki.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoani Tanga
,Kamanda Edward Bukombe amesema ni kweli ajali hiyo imetokea ikihusisha basi
la kampuni ya Tahmeed ambalo lilikuwa likitokea Mombasa kwenda Dar es
Salaam.

Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo,Kamanda Bukombe alisema kwa taarifa
za awali ni hizo hivyo wanaendelea kufuatilia na baadae atatoa
taarifa rasmi kuhusiana na ajali hiyo.


No comments: