Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

TAKUKURU YAWANASA WATUMISHI FEKI WA ‘IKULU’

Tokeo la picha la takukuru mawasiliano
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imewakamata watumishi feki watatu waliokuwa wakifanya matukio kwa kutumia jina la Ofisi ya Rais Ikulu, kwa kosa la kushawishi kuomba na kupokea rushwa.



Watumishi hao ni Ally Matola Ally, ambaye ni Mfanyabiashara wa Masuala ya Bima katika Kampuni ya Iko-Mark Limited na pia anajihusisha na uuzaji wa nafaka katika maeneo ya Bunju.



Mwingine ni Julius Fredric Chiluba, ambaye anajulikana pia kwa jina la Joseph Philip Chiluba, ni Afisa Magereza Mstaafu, anayejitambulisha kama usalama wa Taifa, wote hao kwa pamoja waliomba rushwa ya shilingi Mil 3 na kupokea kiasi cha shilingi Mil 2.



Kutokana na makosa hayo watuhumiwa wamefikishwa mahakamani leo Februari 2, 2018 na kufunguliwa mashtaka chini ya kifungu cha 18, cha katika mahakama ya wilaya ya Temeke.

ANGALIA HAPA

No comments: