ALIYEANGUKA KWA MAKONDA SIRI YAFICHUKA AMANA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mapya zaidi yanayomhusu yule Mkuu wa Idara ya Ardhi, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Paul Mbembela ambaye mwishoni mwa wiki alianguka baada ya kubanwa maswali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yameibuka ambapo siri imefichuka safari yake ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Amana imedaiwa iliishia njiani.
Amani lilizungumza na mfanyakazi mwenzake ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe ambapo alidai kuwa, Paul baada ya kuanguka na kuwekwa kwenye gari la wagonjwa akipelekwa Amana, njiani aliomba kushushwa ili aendelee na hamsini zake.
Mfanyakazi huyo alidai kuwa, wao wameshindwa kuamini kama Paul kweli alipata mshtuko au aliamua kuua soo la kuendelea kuhojiwa maswali na Makonda.
“Mbona Paul hakufikishwa huko Hospitali ya Amana alishukia njiani na anaendelea na maisha yake kama kawaida.
Paul Mbembela akiwa mahtuti.
“Unajua kiukweli tunashindwa kuelewa kama kweli alipata mshtuko au laa, maana alipoingia tu kwenye gari la wagonjwa, akaomba kushuka bila hata kupewa huduma yoyote,” alisema mfanyakazi huyo.
Baada ya habari hizo, Amani liliingia kazini kufuatilia suala hilo ambapo lilianzia Hospitali ya Amana na kufanikiwa kuzungumza na baadhi ya madaktari ambao waliweka wazi kuwa hawajampokea mgonjwa wa aina hiyo.
“Huyo mgonjwa hatujampokea kabisa hapa na hata kama angefikishwa kwa ishu ya kuanguka angeondoka haraka tu si wa kulazwa sana hospitali,” alisema daktari mmoja.
Baada ya daktari kuongea hayo, Amani lilienda Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kumtafuta Paul ili kuongea naye ambapo ilielezwa kuwa hakufika kazini lakini waandishi wetu walifanikiwa kupata namba yake na kuzungumza naye.
Hata hivyo, baada ya kupokea simu, aliitikia vizuri salamu lakini alipoambiwa kwamba unazungumza na mwandishi wa habari, alijibu kwa kifupi na kukata simu.
Amani: Halo nazungumza na Mr Mbembela?
Mbembela: Yeah, nani mwenzangu.
Amani: Naitwa (jina la mwandishi).
Mbembela: Ndiyo bwana niambie.
Amani: Bwana pole sana kwa matatizo yaliyotokea.
Mbembela: Asante bwana kwani wewe umesema ni (anataja jina moja la mwandishi) nani?
Amani: (Mwandishi anarudia kutaja jina lake kamili na kujitambulisha chombo anachotoka) nilitaka kujua unaendeleaje na…
Mbembela: Bwana mimi bado naumwa, niko hospitali na daktari wangu amenikataza kuzungumza kwa sasa.
Amani: Lakini tulitaka kuju…
Mbembela alikata simu na hata alipopigiwa mara kadhaa tena, hakupokea.
Mbembela alizua gumzo la aina yake baada ya kuulizwa maswali na Makonda katika mkutano wake wa kutatua kero mbalimbali za wananchi uliowakutanisha wakuu wa idara zote za Jiji la Dar pamoja na wanasheria katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kwenye mkutano huo, Mbembela alipokuwa akielezea kesi za migogoro ya ardhi zilizopo katika wilaya yake alisema zipo 139 wakati Makonda alisema taarifa aliyonayo yeye ni kesi 1503 na alipobanwa zaidi, ghafla Mbembela alianguka.

No comments: