Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

DIWANI CHADEMA AUAWA USIKU MOROGORO

Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Taarifa za awali zinasema kuwa usiku huu umeme ulikatika katika nyumba yake. Luena akatoka nje kutizama kama kuna shot maana nyumba za jirani zilikuwa na umeme. Alipozunguka nyuma ya nyumba yake kukagua umeme akalutana na kikosi cha watu wenye mapanga wakamkatakata hadi wakamtoa roho.

Ameandika Mbunge wa Mikumi @professorjaytz ameandika;
“Diwani wetu wa Chadema Kata ya Namwawala, Jimbo la MLIMBA (MOROGORO) GODFREY LUENA ameuawa usiku huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana, ðŸ˜­ðŸ˜­ðŸ˜­R.I.P. LUENA.”

No comments: