Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

HAPA NDIPO ATAKAPOZIKWA AKWILINA

KUFUATIA kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwilini ambaye mwili wake umeagwa leo katika viwanja vya chuo hicho na kusafirishwa kwa mazishi, Global Publishers imeshafika nyumbani kwao na marehemu wilayani Rombo-Mashati na kushuhudia maandalizi ya kaburi ambamo atazikwa marehemu.
Maandalizi ya kuchimba kaburi hilo yamefanywa na ndugu na jamaa katika shamba la makaburi ya familia yao yaliyopo kijini kwao.
Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.
 

Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho yua marehemu. AMEN!

NA GPL

No comments: