MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE APIGWA NA WALIMU HADI KULAZWA HOSPITALI
NB- Picha haihusiani na habari hapa chini |
Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo, Bi. Phily Muhebi mkazi wa Kilosa amesema kuwa mwanaye alijeruhiwa vibaya kwa kipigo kutoka kwa waalimu hao Machi 19, mwaka huu kwa kosa aliloelezwa na wanafunzi wenzake kuwa ni baada ya mwenzake mmoja kulalamika kwa walimu kuwa amempaka upupu.
Taarifa za kujeruhiwa kwa mtoto huyo zimefikishwa Polisi huku Mama huyu akilalamikia vitisho alivyopewa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo licha ya mwanaye kuumizwa vibaya na walimu wake.
Mama wa Mtoto huyo amesema kwa sasa anahangaikia matibabu ya mwanaye huyo huku akihofia uwezo wake wa kumudu gharama za matibabu, ambapo ameiomba Wizara ya Elimu kuingilia kati suala hilo sambamba na kuwezesha upatikanaji wa haki dhidi ya unyama aliofanyiwa mwanaye.
Uchunguzi wa Afya mtoto huyo unaendelea, huku taasisi ya mifupa MOI ikiiahidi kutoa tarifa kamili punde baada ya uchunguzi wa kina wa kitabibu wanaoufanya utakapokamilika.
EATV
No comments: