VYETI VIPIMO VYA MASOGANGE VYAVUJA!
WAKATI akitimiza siku tatu kaburini, kijijini kwao, Utengule-Usongwe, Mbalizi jijini Mbeya, vipimo vya afya ya aliyekuwa video queen na msanii wa sinema za Kibongo, Agness Gerald Waya almaarufu Masogange, vimevuja, Ijumaa limedokezwa.
Masogange alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar kwa kile kilichoelezwa na daktari kuwa alilazwa hospitalini hapo kwa siku nne akisumbuliwa na Nimonia na upungufu wa damu mwilini.
MAMBO MENGI YAIBUKA
Mara baada ya kuaga dunia, kuliibuka mambo mengi kwenye mitandao ya kijamii juu ya kifo chake huku magonjwa mbalimbali yakitajwa, lakini kwa waliomjua Masogange vizuri Masogange ndiyo wamemwaga ushahidi wa vipimo vya vyeti vyake vya Ugonjwa wa Ukimwi.
CHETI CHA KWANZA
Kwa mujibu wa vipimo hivyo ambavyo inaonekana alifanya mara mbili kwa nyakati na hospitali tofauti, cha kwanza kinaonesha kwamba, alifanya zoezi hilo, Septemba, 2016 kisha kuyaanika majibu yake kuwa alikuwa HIV-Negative, yaani hakuwa na Ukimwi.
Cheti hicho kilionesha kwamba, Masogange alifanya zoezi hilo la upimaji kwenye Hospitali ya TMJ-Mikocheni jijini Dar. Kwa mujibu wa watu hao wa karibu, Masogange alichukua uamuzi huo kufuatia kuwepo kwa maneno mengi mitandaoni yaliyomhusisha na ugonjwa huo hivyo alitaka kuwakata ngebe waliokuwa wakichonga na kumharibia michongo yake ya mjini.
Taarifa hizo zilionesha kuwa, Masogange alichukua hatua hiyo siku chache baada ya video queen mwingine wa Bongo, Tunda Sebastian kufanya hivyo na kuweza kumaliza kabisa uvumi huo baada ya kubainika kuwa hawana Ukimwi.
CHETI CHA PILI
Kama hiyo haitoshi, ili kumaliza kabisa uvumi huo, Masogange alipima kwa mara nyingine kwenye Hospitali ya Mama Ngoma na kuanika vyeti vya majibu yake kuwa alikuwa HIV-Negative kwa mara nyingine. Duru za kihabari zilionesha kuwa, baada ya kuaga dunia hivi karibuni, madai hayo yaliibuka kwa mara nyingine hivyo kuwapa jukumu watu wake wa karibu kumtetea kuwa alikuwa salama.
MASOGANGE ALIKUWA SALAMA
Katika kumtetea huko ndipo walipojikuta wakianika vyeti hivyo vyote vilivyoonesha kuwa, Masogange alikuwa salama.
“Kiukweli nimeviona vyeti vyake vyote viwili, alikuwa salama kabisa hivyo watu waache maneno kwani kila kitu kinapangwa na Mungu, tumwache Aggy (Masogange) apumzike,” alisema mmoja wa waliokuwa marafiki wakubwa wa mwanadada huyo.
Masogange alianza kupata umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya kwanza ya My Lady ya msanii wa Bongo Fleva, Suma Rider.
UMAARUFU
Baadaye alipata jina zaidi kufuatia kuonekana kwenye video ya Masogange (Macho Yangu) ya Mwanamuziki, Abednego Damian ‘Belle 9’ kisha Msambinungwa ya Tunda Man.
Masogange ameacha mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 11 aliyezaa na jamaa aitwaye Sabri Shaban, mkazi wa Magomeni jijini Dar.
NA GPL
No comments: