MAGUFULI: CHADEMA WATAKIONA CHA MTEMA KUNI
JOHN Pombe Magufuli, rais wa Tanzania amesewaonya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliotangaza kuongoza maandamano kuanzia 1 Septemba mwaka huu,
Rais Magufuli ambaye alikabidhiwa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) siku sita zilizopita, ameanza ziara ya kufanya mikutano ya hadhara katika mikoa mbalimbali kama ilivyotarajiwa ambapo leo alikuwa mkoani Singida.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wilayani Manyoni, Singida Magufuli amenukuliwa akijibu tamko lililotolewa juzi na Chadema kwa kusema, hatua kali zitachukuliwa kwa viongozi hao wa Chadema.
“Wale wanaotangaza kufanya maandamano, watangulie wao wenyewe halafu watakiona cha mtema kuni. Mimi nataka watangulie wao wasiwatangulize watoto wa masikini,” amesema Rais Magufuli huku akiongeza kuwa;
“Wao wanakaa gesti (nyumba za kulala wageni) halafu wanawapa viroba watoto wa masikini ili watangulie kuandamana, sasa mimi nataka watangulie wao halafu waone.”
27 Julai mwaka huu, Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema taifa alitangaza kuwa chama hicho kitafanya mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima ili kupinga kile alichokiita udikteta wa serikali ya awamu ya tano.
No comments: