ANGALIA PICHA::KINGUNGE, MKEWE TANGU UJANA HADI KABURINI
Kingunge na Peres enzi za ujana wao.
KUFUATIA kifo cha mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya taifa Muhimbili, picha za ujana za mzee huyo na mkewe Mama Peras Kingunge zilizotolewa na familia zinaonesha jinsi gani wakongwe hawa walikuwa na mapenzi ya dhati na kuvumiliana tangu ujana wao mpaka umauti unawafika.
aliyekuwa mtumishi wa umma kwa zaidi ya miaka 50 amefariki dunia alfajiri ya Februari 2, 2018 ikiwa ni mwezi mmoja tangu mkewe Mama Peras Kingunge afariki Januari 4, 2018.
Kingunge na Peres uzeeni.
Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 na aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikali ikiwa ni pamoja na kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalumu, mshauri wa Rais Benjamin Mkapa.
Mbali na nafasi hizo serikalini Marehemu Kingunge ameshika nafasi mbalimbali ndani ya Chama cha Mapinduzi -CCM kabla ya kujiondoa ndani ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
No comments: