Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

ASLAY, MSAGASUMU KUTOA ‘MSHIKO’ KWA WAPENDANAO KESHO


MFALME wa Singeli, Selemani Jabir ‘Msagasumu’ pamoja na mkali wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka wanatarajiwa kutoa zawadi ya pesa ‘mshiko’ kwa wapendanao watakaotoka chicha kesho katika Sikukuu ya Valentine’s Day ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akipiga stori na safu hii, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, wasanii hao watakuwa karibu na wapendanao wote watakaoingia ukumbini hapo.

“Njoo ukiwa umependeza na mwandani wako, Dar Live tumewaandalia zawadi kibao kabambe kwa wale watakaopendeza basi watazawadiwa zawadi kibao ikiwemo mshiko,” alisema KP Mjomba.

Naye Aslay aliongeza kuwa, usiku huo mashabiki watapata kusikia ladha ya muziki wa mapenzi akipiga kwa mara ya kwanza ‘live band’.

“Njooni tucheze wote nyimbo zangu za mapenzi zote kuanzia Subalkheri Mpenzi, Natamba, Usiitie Doa, Mahabuba, Baby, Likizo na nyingine nyingi,” alisema Aslay.

Mbali na uwepo wa Aslay na Msagasumu, siku hiyo jukwaa litatawaliwa na Kundi la Taarab, Jahazi Modern huku kiingilio kikiwa 10,000 tu getini.

No comments: