FAIZA AANIKA SIRI ZA WANAUME ALIOZAA NAO
MWIGIZAJI wa Bongo Movies ambaye ni miongoni mwa mastaa wenye wafuasi wengi kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Faiza Ally ameanika siri za wanaume aliozaa nao kwamba, wakati wa ujauzito wa watoto wao walikuwa wakimlea kama malaika kwa sababu walihitaji watoto na walikuwa tayari kuwa na familia.
Faiza aliiambia Risasi Vibes kuwa, akianza na ujauzito wake wa kwanza wa mwanaye Sasha aliyezaa na mwanamuziki ambaye pia ni mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, alikuwa akimlea vizuri kuliko kawaida na hata aliyezaa naye mtoto wa pili anayejulikana kwa jina la Peter, raia wa Marekani naye alikuwa akimpa malezi bora ndiyo maana alifanikiwa kuzaa watoto wazuri.
“Kutokana na malezi mazuri ambayo nimekuwa nikiyapata wakati wa ujauzito, kiukweli ninahamasika kuendelea kuzaa kwa sababu huwa ninalelewa kama malkia, jambo ambalo linanishangaza kusikia wanaume wengine wanawapiga wanawake wao wawapo wajawazito,” alisema Faiza.
No comments: