Jeneza lenye mwili wa Akwilina likiwekwa kaburini.
MWILI wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umezikwa nyumbani kwa wazazi wake kijiji cha Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
Akwilina leo Februari 23, 2018 saa 8:45 mchana huku mamia ya waombolezaji baada ya kumalizika kwa ibada ya mazishi iliyofanyika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Theresia, Parokia ya Olele.
Mwili wa Akwilina uliagwa jana Alhamisi katika viwanja vya NIT vilivyopo Mabibo, Dar es Salaam na kusafirishwa kwenda kijini kwao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Akwilapo akiweka mchanga.
Mwanafunzi huyo alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Jeneza likipelekwa eneo la kaburi kwa kuzikwa.
Akwilina enzi za uhai wake.
picha na GPL
No comments: