JOH MAKINI AFUNGUKIA KUPOTEZWA KIMUZIKI
MWANAMUZIKI ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake uitwao Mipaka, John Simon ‘Joh Makini,’ amefungukia kupotezwa kimuziki na baadhi ya wanamuziki wanaofanya vizuri kwamba si kweli, bali wanaosema hivyo hawafuatilia vizuri muziki wake.
Akichonga na Full Shangwe, Joh alisema kwamba kabla ya watu kuzungumzia juu ya kupoa kwake kimuziki, tofauti na kipindi cha nyuma inabidi waangalie kazi anazofanya na nini kilimfanya asikike sana kuliko wakati huu.
“Si kweli kwamba nimepoa kama ambavyo watu wanakuwa wanazungumza huko kwenye mitandao, mimi bado nipo vizuri na kazi zangu zinafanya poa, zaidi sitegemei kuchuja hata siku moja,” alisema Joh.
No comments: