KAMATI YA NIDHAMU YAMFUNGIA MWAMUZI KUCHEZESHA SOKA
Sehemu ya taarifa ya FFF imeeleza kuwa, ''Baada ya kumsikiliza Tony Chapron na kusoma ripoti ya kamisaa wa mchezo, kamati imeamua kumfungia kwa muda wa miezi sita, pamoja na wiki tatu ambazo alisimamishwa".
Disemba mwaka jana kwenye mchezo wa Ligue 1 kati ya Nantes dhidi ya PSG Chapron alikwatuliwa kwa bahati mbaya na mchezaji wa Nantes Diego Carlos lakini alilipiza kwa kumkwatua mchezaji huyo kisha kumwonesha kadi ya pili ya njano.
Baada ya mechi Tony Chapron alisimamishwa kabla ya usiku wa kuamkia leo kamati ya nidhamu kutangaza kumfungia miezi sita mwamuzi huyo ambaye amechexzesha mechi zaidi ya 400 za Ligue 1 tangu mwaka 2004.
Kabla ya tukio hilo Chapron mwenye miaka 45 alikuwa ametangaza kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho kama mwamuzi na alitarajia kustaafu mwishoni mwa msimu wa 2017/18.
No comments: