MATUKIO YA UCHAGUZI KINONDONI NA SIHA
Saa 2:00, Asubuhi:
ZOEZI la upigaji kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani katika baadhi ya maeneo, Tanzania Bara limeanza limeanza rasmi asubuhi hii ya leo tarehe Februari 17, 2018 ambapo majimbo mawili ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro yatakuwa kwenye mchakato wa kuwachagua wabunge wao baada ya waliokuwepo kujiuzulu.
Vile vile, uchaguzi huo utafanyika kwa Madiwani katika Kata nane Tanzania Bara na kuhusisha wapiga kura 355,131 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kutakuwa na vituo vya kupigia kura 867.
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema leo asubuhi saa 2:00 huku wananchi wakijitokeza kuchagua viongozi wawakilishi wao na ulinzi ukiwa umeimarishwa na jeshi la polisi.
Katika Jimbo la Kinondoni, Said Mtulia wa CCM anachuana na Salum Mwalimu wa Chadema ambapo Siha, Elvis Christopher Mosi wa Chadema akichuana na Dkt. Godwin Ole Mollel wa CCM.
Saa 2:10, Asubuhi:
Wananchi wameendelea kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Kinondoni katika Eneo la Mwenge Dar es Salaam, ambapo wamesema zoezi hilo linaenda vyema toka vituo vilipofunguliwa asubuhi hii leo.
Saa 2:30, Asubuhi: Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM Maulid Mtulia amepiga kura katika kituo cha Friends Corner, Kata ya Ndugumbi nakusema zoezi hilo limekwenda salama. Amesema atakubaliana na matokeo yoyote yatakayo tangazwa.
Saa 3:15, Asubuhi:
Siha: Mawakala 67 kati ya 70 wa Chama cha Wananchi (CUF ) wanaosimamia uchaguzi mdogo Jimbo la Siha wametolewa vituoni kwa madai kuwa barua zao za kiapo zimesainiwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo pekee badala ya kusainiwa na hakimu.
Saa 4:00, Asubuhi:
Kinondoni: Kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi Mwongozo katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura ni ndogo.
No comments: