BABU MBARONI KWA KUGUSHI VYETI, AKUTWA NA MIHURI 54 YA MAGUMASHI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limamshikilia Selemani Masoud (60) mkazi wa Yombo Kialakala kwa tuhuma za kutengeneza vyeti vya kugushi vya vyuo na taasisi mbali mbali za za serikali, nyaraka za serikali na mihuri bandia.
Hayo yamesemwa leo, Ijumaa, Machi 16, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.
“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa chanzo chetu, tulimkamata mtuhumiwa na kufanya upekuzi nyumbani kwake, tulikuta nyaraka mbalimbali na jumla ya mihuli 53, nyaraka za Necta, mihuli ya Veta, UDSM, Chuo cha Bandari, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, SUA, Mtwara Universirty, Mkuu wa Chuo Cha UDSM, TRA, NIT, IFM, Bodi ya Taifa ya Bandari (NBAA), Tumaini University (TUDARCO), Mwl Nyerere Univesity, RITA, JKT Makao Makuu, Mahakama ya Kisutu, Chuo cha Uhasibu Arusha, Msajili wa Ndoa, Shule za Sekondari, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na vingine,” alisema Mambosasa.
Pia amekutwa na vifaa vya Kompyuta, Cheti cha Elimu Uganda, Mzumbe University, stika za Necta na vingine ambapo mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakani upelelezi utakapokamilika.
No comments: