Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

KAULI YA DIAMOND KUHUSU NDOA YA ALI KIBA

Ikiwa  msanii Alikiba ameoa hapo jana , mshindani wake kimuziki Diamond Platnumz hajakaa kimya kwenye hilo.

Diamond amefunguka kuwa amepewa taarifa za Alikiba kuoa siku ya jana , hivyo amemtumia salamu na kumtakia maisha mema ya ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Intagram tumegulia kile alichogusia kuhusiana na ndoa ya Alikiba;

"Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥 " ameandika  Diamond.

Msanii Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake  Aminah Rekish  mjini Mombasa nchini Kenya

No comments: