MBUNGE ANA MAJINA YA WALIMU MADUME YA MBEGU, WAPENDA NGONO
Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga amewachongea walimu wanaume wanaodaiwa kupenda kuomba rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike, kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Mlinga ameyasema hayo bungeni leo Aprili 30 wakati akichangia mjadala wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Akikumbushia mada yake ya wiki iliyopita, Mlinga amesema, “Taarifa niliyoipata kutoka kwa Waziri wa Elimu alisema hakunielewa vizuri na waheshimiwa wabunge mtakuwa mashahidi.
“Kumekuwa na tatizo la vyuo vikuu wanafunzi wetu wa kike wanapata shida mno, katika vyuo vyetu kuna walimu wanaojulikana kabisa kwamba hawa walimu ni madume ya mbegu, wanafelisha wanafunzi wa kike wanataka wawape rushwa za mapenzi ndiyo wawafaulishe.
Mheshimiwa Waziri nitashirikiana na wewe kama utanipa ushirikiano nitakueletea majina ya vyuo vikuu vyote Tanzania na walimu madume ya mbegu ambao kazi yao ni kufelisha wanafunzi na kutaka rushwa za ngono.” Amesema Mlinga.

No comments: