MWENYEKITI PAC AWAKOSOA MAWAZIRI WA JPM
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka amesema si sahihi mawaziri kujibu taarifa ya ukaguzi ya CAG.
Akizungumza bungeni leo Aprili 16, bungeni, Kaboyoka amesema kilichofanyika sasa ni makosa kwa sababu ukaguzi huo umefanyika mwaka 2016/17.
Amesema kama ni ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha si sahihi waziri kueleza kuwa fedha zilizopotea zimeanza kulipwa, wakati ubadhirifu huo umefanyika mwaka 2016/17.
“Sasa leo tuhoji jambo moja, kama fedha hizo zimepotea hizi wanazoanza kulipa sasa wamezitoa wapi. Kama kulikuwa na cheni ya ulaji tutaijuaje. Hicho ndio kitu cha msingi. Hoja za CAG zinapaswa kujibiwa na maofisa masuhuli na kurudishwa tena kwa CAG ili ahakikishe kama kilichojibiwa ni sahihi,” amesema Kaboyoka.
Wiki iliyopita mawaziri waliitisha mkutano na wanahabari kujibu hoja zilizoibuliwa katika ripoti ya CAG.
No comments: