OFISA AJIUA KWA KUJITUNDIKA KAMBA ZIZINI
Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Michael Fundo (57), amefariki dunia kwa kunywa sumu kabla ya kujitundika kwa kamba ndani ya zizi la ng’ombe nyumbani kwake wilayani Misungwi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo linalodaiwa kusababishwa na msongo wa mawazo kutokana na Michael kuwa na ugomvi wa muda mrefu wa kifamilia.
Mmoja wa wanafamilia aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amesema ugomvi huo ulitingisha pia ndoa yake.
“Kabla ya kujinyonga kwa kamba, alikunywa sumu aliyoona inamchelewesha,” amesema Kamanda Msangi.
Licha ya kuwa mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana ambayo kwa pamoja na Ilemela zinaunda Jiji la Mwanza, Michael alikuwa akiishi wilaya jirani ya Misungwi.
Mtumishi wa ndani wa familia hiyo, John Anthony (23) amesema kabla ya kuchukua uamuzi wa kujitoa uhai, alifanya hesabu ya kikundi cha kuweka na kukopa ambacho alikuwa mtunza fedha na kukabidhi nyaraka na fedha zote akielekeza zikabidhiwe kwa wana kikundi wenzake.
“Marehemu pia aliandika wasia ukihusisha mali pamoja na madeni anayodai na kudaiwa, jambo lililotutia mashaka ni kwa nini anafanya hivyo,” amesema Anthony.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanakikundi, leo Aprili 28, walipanga kugawana fedha walizokusanya.

No comments: