Header Ads

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

RIDHIWANI KIKWETE ALAANI MAUAJI YA MDOGO WAKE HECHE

Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amelaani kitendo kilichofanywa na askari polisi E.115 Koplo William Marwa anayetuhumiwa kumuua kwa kisu Suguta Marwa (27), mkazi wa Kijiji cha Sirari wilayani Tarime mkoani Mara.





Suguta ambaye ni mdogo wa mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche inaelezwa aliuawa usiku wa kuamkia jana Aprili 27, 2018 huku Kamanda wa Polisi Kanda ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe akisema Marwa anamshikilia kwa uchunguzi zaidi.





Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete amelaani tukio hilo akisema, “kitendo kilichotokea sio tu kimesikitisha ukoo wa Bwana Heche lakini kwangu binafsi.”






“Jeshi letu limetengenezwa kulinda watu na mali zao sio kuumiza wasio na hatia. Ni imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya Heche. Poleni sana kwa msiba. Mungu awape subira,” ameongeza Ridhiwani ambaye katika mahojiano na MCL Digital amekiri ujumbe huo kuwa ni wake.

No comments: