WAZIRI ABANWA UHABA WA MAFUTA
Suala la amfuta ya kula limetikisa bunge huku Spika wa bunge Job Ndugai , akimwagiza waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji Charles Mwijage ,kuandda na kuwasilisha bungeni jijini Dodoma majibu ya uhakika kuhusu tatizo hilo.
Ndugai alitoa kauli
hiyo baada ya wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
George Lubeleje
(Mpwapwa) na Hussein Bashe (Nzega Mjini) kuliibua tena sakata hilo bungeni jana
asubuhi.
Mara tu baada ya
kumalizika kwa kipindi cha 'Maswali', wabunge hao walisimama na kuomba mwongozo
wa Spika kuhusu kile walichodai kupanda kwa bei ya mafuta ya kula nchini
kutokana na kuzuiwa kwa meli za mafuta zinazodaiwa kuwa na mafuta ghafi kwenye
Bandari ya Dar es Salaam.
Katika kujenga hoja
yake, Lubeleje alisema mbali na nchi kukabiliwa na uhaba wa sukari, baadhi ya
vyombo vya habari vimeendelea kuripoti kuhusu upungufu wa mafuta ya kula huku
wenye viwanda wakisitisha uzalishaji kwa kukosa mafuta ghafi.
"Sasa, Waziri wa
Biashara anasemaje kama tukikosa mafuta ya kula nchi nzima, tufanye
nini?," alisema Lubeleje ambaye kwa sasa ndiye mbunge mkongwe zaidi
nchini.
Hoja hiyo iliungwa
mkono na Bashe ambaye alidai bei ya mafuta aina ya Korie imepanda kutoka Sh.
23,000 hadi 40,000 kwa ndoo ya lita 10 na kwa ndoo ya lita 20 imepanda kutoka
Sh. 50,000 hadi 73,000.
“Kuna haja ya kutoa
mwongozo serikali ije na kauli rasmi kuhusu hii 'crisis' (janga) ya mafuta na
sukari. Tunafanya nini kama nchi kuweza kumpunguzia mzigo mwananchi?"
Bashe alihoji na kuongeza:
"Ongezeko la bei
ni zaidi ya asilimia 20 kwa kipindi cha miezi mitatu wakati waziri jana (juzi)
alisema bado upimaji unaendelea kati ya taasisi yaani TBS (Shirika la Viwango),
Mkemia Mkuu wa Serikali na UDSM (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam)."
Katika mwongozo wake
kwa wabunge hao, Spika Ndugai alisema kuwa licha ya waziri kutoa maelezo,
anaona hayatoshelezi hivyo akamtaka kuandaa majibu mazuri zaidi na kulieleza
Bunge kuhusu suala hilo.
Awali akitoa ufafanuzi
bungeni kuhusu sakata hilo, Mwijage alisema ni vyema Watanzania wakaelewa
vizuri kuhusu ongezeko la uhaba wa mafuta.
"Tanzania
tunazalisha mafuta kutokana na mbegu mbalimbali zikiwamo alizeti, karanga ufuta
na pamba, kiasi hicho hakikidhi mahitaji," alisema.
Aliongeza kuwa mbegu
hizo zinazalisha mafuta kwa asilimia 30, lakini pia sehemu ya kiasi hicho
hususani ya mafuta ya alizeti inauzwa nchi za nje kutokana na kuwa na mahitaji
makubwa.
"Ili kukidhi
mahitaji ya nchi, huagizwa mafuta kutoka nje ambayo ni mafuta ghafi na
yaliyosafishwa kutoka nchi za Indonesia na Malaysia," Mwijage alisema na
kueleza zaidi:
"Mafuta ghafi
yakiingizwa nchini, sheria ya Tanzania hutoza asilimia 10, wakati Kenya hutoza
asilimia sifuri, tukiwa tunalenga kuwapa faida wazalishaji wa mbegu wa Tanzania
kupata faida na viwanda viweze kusimama."
Waziri huyo
alibainisha kuwa tatizo lililoleta shida ni mafuta tani 40,000 yaliyopo ndani
ya matenki na meli zilizopo nje kuwa na utata kwenye vipimo.
"Wataalamu wetu
walipoyapima kuna nyaraka zinasema ni mafuta ghafi, kuna zinazosema si ghafi,
mtoza ushuru anasimama katikati, sasa yakiingia nchini tukisema si ghafi,
serikali itapoteza ushuru wa Sh. bilioni 22," alisema.
Aliongeza:
"Ikaundwa kamati chini ya wizara yangu, kujua ni kipi, haichukui mwaka kupima
ila vipimo vya watalaamu ndiyo vimemsababisha mtoza ushuru (TRA) awe na
mashaka."
Mwijage alisema
alizungumza na watalaamu wanaohusika kuhusu suala hilo, hivyo anaamini
wataalamu watakuja na majibu.
Alisema alishatoa
ushauri kwa TRA na wenye mafuta lakini hawakukubaliana nao, akieleza kuwa
katika ushauri huo alitaka nusu ya mzigo ushushwe kwa makubaliano.
"Tunalazimika
kuhakikisha kila shilingi inakusanywa, sasa wale waokusanya wanapopata mashaka
inakuwa shida, tunalifuatilia na wahusika nipo nao ili kila upande upate haki.
Nimekuomba kabla ya
saa 11 jioni (jana) nirudi kuja kukupa majibu," alisema Mwijage.
KUBANGAIZA
Baada ya waziri kutoa
ombi hilo, Spika Ndugai alilikubali lakini akasisitiza ni lazima serikali
iwasilishe majibu bungeni jana jioni.
"Bahati nzuri
nitakuwa hapa (kwenye Kiti cha Spika), ni utamaduni duniani kote. Tunapokuwa
bungeni lazima tuseme ukweli, tukigeuza Bunge kuwa mahali pa kubangaiza,
haitakuwa sawasawa. Kwa hiyo, saa 11 tuje na maelezo ya jambo hilo," Spika
Ndugai aliagiza.
Kiongozi huyo wa Bunge
pia alimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira, Sadick Murad, kueleza kilichojiri wakati kamati hiyo ilipokutana na
TBS.
Kutokana na agizo
hilo, Murad alisima na kueleza kuwa walikutana Jumamosi na kuzungumzia suala
hilo wakiwa na watendaji wa wizara, TBS, Tume ya Ushindani (FCC) na Wakala wa
Usajili wa Majina na Leseni za Biashara (Brela).
Alisema kuwa katika
semina hiyo, kulijitokeza suala hilo kuwa zipo meli ambazo kwa zaidi ya wiki
mbili zimezuiwa mkanganyiko wa aina ya mafuta ziliyobeba.
"TBS wamesema ni
mafuta ghafi, Mkemia Mkuu anasema ni mafuta ghafi, TRA wanasema siyo ghafi,
tukauliza TRA wana maabara yao?
"Baada ya kuuliza
hivyo, ikaanza mijadala hadi kufika leo (jana) mafuta yameanza kupanda bei na
viwanda havina mafuta ghafi na bei zimeendelea kupanda. Niombe saa 11 tupate
majibu ya uhakika," Murad alilieleza Bunge.
Kutokana na maelezo
hayo ya Mbunge huyo wa Mvomero (CCM), Spika Ndugai alisimama na kusema anatoa
nafasi kupata ufafanuzi huo ili uhalisia upatikane.
"Mnatukifikisha
mahali pagumu sana kwa mambo madogo sana. Hivi kweli nchi hii leo wale wote
tuliosoma Chemistry kupima mafuta kujua ghafi au safi hiyo ni rocket
science?" Spika Ndugai alihoji.
"Kitu cha dakika
15 watu wanazunguka. Nilisema kama TRA hamwamini Mkemia Mkuu, ana maabara yake,
pelekeni Afrika Kusini, Nairobi (Kenya) au London (Uingereza), dakika chache
majibu unapata, unapiga kodi mambo yameisha.
"kama
ikitengeneza mazingira ya TRA kusema mbabe mmoja anasema, haiwezi kuwa hivyo
kwani mafuta hayo kusalia bandarini yatakapoingia
mtaani atakayelipia ni mwananchi wala siyo matajiri.
mtaani atakayelipia ni mwananchi wala siyo matajiri.
NIPASHE
No comments: