BUNGE LAZUIA WAZIRI MKUU KUJIBU SWALI WARAKA KKKT
Uongozi wa Bunge jana ulimzuia waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujibu swali na mbunge wa upinzani kuhusu serikali kulipa siku 10 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani (KKKT)
...kufuta waraka wake wa Pasaka uliotolewa Machi 24, mwaka huu, kwa maelezo kuwa linagusa masuala ya kidini ambayo Spika Job Ndugai ameshazuia kuhojiwa bungeni.
Kutokana na uamuzi huo, wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), waliitisha mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Elimu ya Bunge, jijini hapa na kueleza kuwa vitaendelea kuibana serikali bungeni kuhusu suala hilo huku vikiyataka makanisa ya KKKT na Katoliki (RC) yasijibu barua yalizopewa na serikali.
Ukawa unaundwa na Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi na NLD.
Swali kuhusu KKKT iliyoandikiwa barua ya kutakiwa kufuta waraka huo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, liliulizwa bungeni jijini Dodoma jana na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) wakati wa kipindi cha 'Maswali kwa Waziri Mkuu'.
Katika swali lake, Mbatia alitaka kujua ukweli kuhusu barua zinazodaiwa kuandikwa na serikali kwenda kwa makanisa hayo.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, aliitaka serikali kueleza uamuzi huo una lengo gani.
"Kuna barua wamepewa KKKT na TEC (Baraza la Maaskofu Katholiki Tanzania) wakitakiwa kufuta nyaraka zao za Kwaresima," Mbatia alisema.
Hata hivyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, aliyekuwa anaongoza kikao cha jana, alizuia swali hilo kujibiwa akieleza kuwa tayari Spika Ndugai ameshatoa maelekezo kwa maswali ya aina hiyo.
"Mtakumbuka Mheshimiwa (Saed) Kubenea (Mbunge wa Ubungo-Chadema) alimwuliza Waziri Mkuu swali linalohusu dini na Mheshimiwa Spika alizuia suali hilo kujibiwa,” alisema.
Dk. Tulia alisema kisha akatoa nafasi kwa mbunge mwingine kuuliza swali kwa Waziri Mkuu huku Mbatia akilazimika kuketi na kuanza kujadiliana na wabunge wengine wa vyama vya upinzani waliokuwa karibu naye.
TAMKO LA UKAWA
Baada ya kumalizika kwa kipindi cha 'Maswali' bungeni, wabunge wa Ukawa walizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari ya Bunge, wakiziomba KKKT na TEC kutojibu barua zilizopewa na serikali.
Pia waliitaka serikali kuwaomba radhi waumini wa madhehebu hayo huku wakieleza kuwa kuanzia jana watahakikisha wanatumia mbinu mbalimbali ndani ya Bunge kuitaka serikali kutoa majibu ya kina kuhusu barua hizo na kuibana ili izifute.
Kaimu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Abdallah Mtolea, alisema viongozi wa kiroho wanaaminika kuliko wanasiasa, hivyo kambi yao itahakikisha suala hilo halivurugi nchi.
"Tumeamua kuyasema haya yanayofanyika kwa kuwa yanakwenda kuivuruga nchi hii. Taasisi hizi zinaongozwa na viongozi wa kiroho wanaoaminika kuliko sisi wanasiasa," alisema.
Mbunge huyo wa Temeke (CUF) aliongeza: "Serikali iache kuingilia hizi taasisi, iache kuwaingilia na kusema wanachanganya masuala ya dini na siasa."
Katika mkutano huo, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), alisema serikali inatakiwa kuzifuta barua zake kwenda kwa taasisi hizo za dini.
"Tutahoji na tutatumia kanuni zote za Bunge kuitaka serikali kutoa majibu yake na hili tutalifanya kwa umoja wetu," alisema.
Mnyika ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara, aliongeza: "Kimsingi, serikali inapaswa kuifuta barua hiyo iliyoandikwa na Komba kwa kuwa hili ni kaa la moto kwa serikali."
Naye Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema Waziri Mkuu ndiye msimamizi na mdhibiti wa shughuli za serikali bungeni, hivyo swali aliloulizwa bungeni jana asubuhi kuhusu hatima ya KKKT na RC lilipaswa kujibiwa na kiongozi huyo kwa kuzingatia kwamba ni la kikatiba.
Mwenyekiti mwenza huyo wa Ukawa alisema KKKT ilitoa waraka wa Pasaka na TEC walitoa wa Kwaresima na wote wametakiwa kufuta waraka huo ndani ya siku 10 kuanzia Mei 30, mwaka huu.
"Tunashauri wasiwajibu serikali halafu waone serikali itachukua hatua gani kwani nchi hii si mali ya serikali. Waumini wako katika hamaki, viongozi hawa wa dini ni Watanzania na wana haki ya kutoa maoni. Serikali inapaswa kuwaomba radhi waumini," alisema.

NIPASHE
No comments: